contact


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, November 24, 2011

MIGOMO SIO ISHU

Kwa mtazamo wangu kiukweli mimi sioni faida ya migomo no matter tunapigania kitu gani, hii ni kutokana na mambo yaliotokea hapa juzikati, baaadhi ya wanafunzi wameumizwa kwa kupigwa na askari, wengine tumeumizwa na mabomu ya machozi, hii sio mara ya kwanza kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kugoma na kuandamana, kama kweli migomo ingekua inasaidia, haya matatizo yasingekua yanajirudia, tutaendelea kupigwa mabomu ya machozi na mwisho wa siku tutakuja kupigwa hata na risasi za moto na matatizo yataendelea kujirudia kama kawa, me nashauri tungejaribu kutafuta njia nyingine ya kuwafanya hawa viumbe watuelewe, kuna wanafunzi wa mwaka wa kwanza pia wameandamana, nyie hamjafikisha hata semista moja hapa chuo mmeshaanza kujiingiza matatizoni, mkiumizwa au kufukuzwa chuo mtawaelezea habari gani wazazi wenu ambao wanajinyima ili nyie mpate elimu, acheni kufata mkumbo wadogo zangu, someni, hicho ndicho kilichowaleta UDSM.

Friday, November 4, 2011

CHUO CHA MAENDELEO NA USIMAMIZI WA MAJI (WDMI)

          Jina chuo cha maendeleo na usimamizi wa maji linaweza kuwa geni masikioni mwa watu, lakini chuo hichi ni moja kati ya vyuo vikongwe hapa nchini, kilianzishwa mwaka 1974 kikijulikana kama RWEGALULILA WATER RESOURCE INSTITUTE, dhumuni kubwa ikiwa ni wataalam katika fani mbalimbali zinazohusu MAJI.
         Kubadilika kwa jina na kuwa WATER DEVELOPMENT AND MANADEMENT INSTITUTE, ilifanyika mwaka 2008, baada ya chuo kupewa hadhi ya kuwa wakala wa serikali yaani Agency, mpaka sasa chuo kinatoa kozi tano katika ngazi ya Diploma, WATER SUPPLY AND SANITATION ENGINEERING, HYDOGEOLOGY AND WATER WELL DRILLING. HYDROLOGY AND METROLOGY, WATER LABORATORY TECHNOLOGY na IRRIGATION ENGINEERING. Mipango ya degree kuanza imekamilika na muda wowote WATER RESOURCE AND IRRIGATION ENGINEERING  itaanza, sasa kazi kwenu nyie wenye hamu ya kufanya kazi kwenye sekta ya maji, mnakaribishwa sana.

Monday, October 24, 2011

WANACHUO SJMC KUANDAMANA BODI YA MIKOPO LEO

Licha ya wanafunzi kupiga kelele kibao na migomo ya hapa na pale kuielekea bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania, bodi hiyo inaonyesha live kutozingatia kwa kuendelea kuchelewesha mikopo ya wanafunzi. Hii inatokana na wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma (sjmc) kutopata mkopo wao hadi leo, Wanafunzi wa chuo hicho sasa hivi wameamua kwenda bodi ya mikopo ili wakapate kujua ni ishu gani inaendelea na kwanini haya matatizo hayaishi, ni uzembe tu wa wafanyakazi au inakuaje, tunakoelekea kama tatizo hili litaendelea itakua balaa, Bodi kaeni chonjo mmeshatuchosha

Wednesday, September 21, 2011

UKWELI KUHUSU MIGOGORO YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

Kwa takribani miaka minne sasa, kumekuwepo na mvutano kati ya Taasisi ya ustawi wa jamii (ISW) na Baraza la taifa la Elimu ya juu na ufundi (NACTE), kuhusu masuala ya taaluma katika taasisi hiyo. Mvutano huo uliwasukuma baadhi ya wahadhiri katika taasisi hiyo kushinikiza menejimenti yao kutekeleza mapendekezo ya baraza hilo kuboresha taaluma, lakini kilichowakuta wahadhiri hao, licha ya juhudi zote zilizofanywa na vyombo mbalimbali kujaribu kurekebisha mambo katika taasisi hiyo, bodi ya chuo iliridhia kuwafukuza kazi wahadhiri 21 mnamo agosti 21 mwaka huu, ambao kosa lao pekee kubwa ni kutaka taaluma iboreshwe katika chuo hicho

Wahadhiri hao wamefukuzwa kwa madai kwamba waliendesha mgomo usio halali na kukaidi maagizo ya mamlaka za juu


Mambo bado si shwari katika taasisi hiyo, mpaka sasa hakuna maboresho yoyote ya maana ya kitaaluma yaliyofanyika,  bali kinachoendelea pale ni migogoro ambayo hatma yake ni kuzalisha wahitimu walio chini ya kiwango wasioweza kushindana vyema katika soko gumu la ajira nchini


Ukweli ni kwamba, kiini cha migogoro ni taasisi kuendelea kupuuza maagizo ya NACTE. kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba barua za NACTE zenye kumbukumbu NACTE/ DA/ 31/655/Vol 1./92 ya june 19/ 19/ 2010; zinaonyesha taasisi ya ustawi wa jamii ilipewa maagizo ya kufanya maboresho ili kukidhi matakwa ya ithibati yanayokubalika NACTE

Kwa mshangao, menejimenti iliamua kukaidi maagizo hayo ya NACTE. Na hili ndilo pia lililosababisha wahadhiri watatu waandamizi wa chuo hicho -Dk Mihanja, Dk Matiku na Dk Kitojo kujiuzulu kazi mwaka 2007.


Ukaidi huo ulisababisha taasisi kuzuiliwa kujihusisha na udahili wa programu za ngazi ya cheti, stashahada na shahada (certificate, diploma, degree programs) ilipofika April 2011, kwa kuwa ilishindwa kukidhi matakwa ya ithibati ya kwanza iliyoidhinishwa na NACTE kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2006-2011


Kwa barua hizo taasisi ilipewa muda mpya wa kuandaa mitaala na kurekebisha mfumo wa utawala hadi ifikapo septemba 2011 ili warudishiwe haki ya kuendesha program hizo, mpaka wiki mbili zilizopita hilo lilikuwa halijatendeka

Kwa ufupi, si kweli kwamba tatizo la taasisi hiyo lilikua ni hao wadhahiri waliofukuzwa kazi kama inavyodaiwa, wao walikuwa wakipigania taasisi hiyo kutii maagizo yaliyotolewa na NACTE. Si kweli kwamba waliachishwa kazi kwa kufanya mgomo usio halali, na si kweli kwamba kwa kuwafukuza kazi, hali ya kitaaluma ya taasisi hiyo itaboresheka,  ni mpaka hapo hilo litakapozingatiwa, hali ya kitaaluma ya taasisi hiyo haiwezi kuwa shwari, kwa sababu wahitimu wa taasisi hiyo wataendelea kuwa chini ya viwango na ajira zitaendelea kuwakimbia


menejimenti ya taasisi hiyo imekiuka haki za msingi za wafanyakazi walioachishwa kazi bila kufuata kanuni za ajira za taasisi ya ustawi wa jamii (staff regulation) na sheria ya kazi Na.6 ya mwaka 2004, na kwa mujibu wa katiba ya nchi, pia imewadhalilisha wadhahiri hao walioachishwa kazi wakipigania maslahi ya taasisi, maslahi ya wanafunzi na maslahi ya umma mzima wa Tanzania

Monday, September 19, 2011

SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA LATEKETEA KWA MOTO

Mbunge wa Mbeya mjini, Mh Joseph Mbilinyi aka Sugu akiwa ametembelea soko la SIDO mwanjelwa jijini Mbeya likiwa linateketea kwa moto

Moto ukizidi kupamba katika soko la mwanjelwa Mbeya mjini,  raia wakikimbia kuokoa maisha yao na wengine wakikimbilia eneo la tukio kuokoa chochote kinachowezekana, chanzo cha moto huu hakijajulikana mpaka sasa

Mabanda ya soko yakiteketea, kikosi cha kuzima moto cha jiji hili kilifika eneo la tukio kuzima moto na kuokoa watu na mali zao kikiwa na gari bovu na pia likiwa halina maji ya kuzimia moto huu

AJALI YA MELI ZANZIBAR

abiria wa meli ya MV Spice Islander ilyopata ajali usiku wa kuamkia septemba 10,2011 ikiwa inaelekea Pemba  kutokea Dar es salaam wakijitahidi kuokoa uhai kwao kwa kutumia magodoro yaliyokuwamo katika meli hiyo

Muonekano wa nje wa meli ya MV Spice Islander kabla ya kupata ajali, meli hii inasemekana ilibeba abiria zaidi ya 1500, idadi ambayo ni zaidi  ya mara mbili ya idadi ya abiria inayopaswa kubeba

Baadhi ya miili ya abiria iliyopatikana katika ajali hiyo, mamia ya watu wamepoteza uhai katika ajali hii

Baadhi ya wahanga wa ajali hii waliofanikiwa kuokolewa

Makaburi yaliyochimbwa Zanzibar kwa ajili ya kuwazika marehemu wa ajali ya meli

Meli ya MV Spice ikiwa imepinduka maeneo ya Nungwi, meli hii iliondoka bandari Zanzibar kuelekea jioni ya tarehe 9 septemba, ilianza kuzama mida ya saa 3 usiku na hatimaye kupinduka  na kuzama kabisa, meli hii ilielemewa na mizigo na idadi kubwa ya abiria

Askari na raia wakijitahidi kuokoa abiria waliosalimika katika ajali hiyo, kikosi cha jeshi la polisi wanamaji KMKM na JKU bado vinaendelea na utafutaji wa miili ya abiria wengine wa ajali hiyo

muonekano  wa meli ya MV spice ikiwa inaendelea kuzama ndani ya maji

Baadhi ya miili ya watoto wadogo waliopoteza maisha katika ajali ya meli

Ndugu na jamaa wakiwaombea watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli Zanzibar. hii ni meli ya pili kuzama ikielekea Pemba, nyingine ni MV Fatahi iliyozama mwaka jana ikiwa bandari zanzibar kuelekea Pemba

Friday, September 9, 2011

MAMILIONI KUMWAGIKA KISIWANI KILWA

shehemu ya mabaki ya kilwa
 Sept 7, 2011 serikali ya Marekani kupitia balozi wake nchini imewasilisha msaada wa (1,132,000,000.00) shilingi za kitanzania, karibia bilioni moja na robo kusaidia utunzaji wa hifadhi za kumbukumbu za Kilwa
ufukwe wa bahari, Kilwa
 Hifadhi hizo  ambazo zimekuwepo tangu karne ya 19 zinatakiwa kutunzwa ili ziendelee kuwa kivutio kizuri cha utalii nchini na kuingizia taifa kipato zaidi. Msaada huo uliopita chini ya US Department of State's Ambassadors Fund for Cultural Preservation (AFCP) umetolewa kwa lengo la kusaidia utunzaji wa hifadhi za mambo ya kale Africa Mashariki na pia kuwawezesha wakazi wa maeneo hayo kunufaika na hifadhi hizo
sehemu ya mabaki ya Kilwa

NIGER KUMSHUGHULIKIA GADDAFI

Col. Muammar Gaddafi
 Serikali ya Niger imesema kuwa itaamua jinsi ya kushughulika na kanali Muamar Gaddafi iwapo ataingia nchini humo kuomba hifadhi ya kisiasa
Kanali Muamar Gaddafi
Ripoti kutoka eneo hilo zimesema maofisa wa  vyeo vya juu katika serikali iliyotimuliwa wamewasili nchini Niger na kuna habari kuwa huenda Gaddafi akajiunga nao. Baraza la mpito la Libya limetoa wito kwa serikali ya Niger isimpe hifadhi kanali Gaddafi
Kanali Gaddafi na walinzi wake wa kike
 wakati huo huo Kanali Gaddafi amepuuza madai kwamba ametorokea nchi jirani ya Niger na kuyataja madai hayo kama uongo  na vita vya kiakili. Matamshi ya Gaddafi yamepeperushwa na kituo kimoja cha TV nchini Sirya kilichodai kuwa Kanali Gaddafi bado yupo nchini Libya. Gaddafi ameapa  kuwashinda wapiganaji wa upinzani wanaoungwa mkono na majeshi ya NATO. Huu ni ujumbe  wake wa kwanza katika kipindi kirefu
Walinzi wa Kanali Gaddafi
.
Baraza la kitaifa la mpito la Libya limetoa wito kwa Niger kutompa hifadhi Kanali Gaddafi. Serikali ya  Niger imesema kwamba itaamua yenyewe jinsi itakavyomshughulikia Gaddafi ikiwa ataingia nchini humo

OBAMA kuwekeza katika elimu tena, KIKWETE......??

raisi Barrack Obama
 Raisi wa marekani Barrack Hussein Obama amewasilisha mpango unaoazimia kufufua uchumi na kutoa nafasi mpya za ajira utakaogharimu dola za kimarekani billion 450
Katika hotuba yake iliyokua ikingojewa kwa hamu, Obama ameliambia bunge la marekani, lengo ni kufufua uchumi wa marekani uliozorota, kutoa nafasi mpya za ajira na kuwapa vijana matumaini
Kiini cha mpango huo ni kupunguza gharama za ruzuku ya serikali kwa wale wasiojiweza na kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu na miundo mbinu, pia ameongeza kuwa atabadilisha mfumo wa kodi uwe ni wa haki kwa kila mmoja
rais Jakaya Kikwete
Raisi wetu kikwete tungependa uige mifano kama hii, kodi  sawa kwa wwote, rasilimali ziwasaidie wananchi wa hali zote na sio wanaojiweza tu na kikubwa zaidi ni kuwekeza katika elimu, walimu ni wachache nao pia kila kukicha wanalalamika mishahara haiwatoshelezi mahitaji yao, wanafunzi wa vyuo vikuu wanagoma kila kukicha wakidai  mikopo, shule  za kata nyingi lakini vitabu hakuna, wakati huo huo mshahara wa mbunge kwa mwezi ni sawa na mshahara  wa mwalimu wa kawaida kwa mwaka mzima

WANAFUNZI WAVAMIA OFISI ZA TCU

wanafunzi wakiwa katika maandamano
 mamia ya wanafunzi ambao hawakuchaguliwa na tume ya vyuo vikuu (TCU) kujiunga na vyuo vikuu nchini juzi walivamia ofisi za tume hiyo ili kufahamu sababu za kutochaguliwa kwao licha ya kuwa na vigezo na sifa zote zinazotahitajika ili kuchaguliwa
wanafunzi wakiwa katika maandamano
Vijana hao ni miongoni mwa wanafunzi 10,553 ambao hawakuchaguliwa kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka huu. Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa na TCU kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka huu imepungua ukilinganisha na ile ya mwaka jana, 

BODI YA MIKOPO KUCHUNGUZA TENA UTOAJI WA MKOPO KWA WALIOKOSA

bodi ya mikopo elimu ya juu
Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania (HELSB) imepewa muda wa wiki mbili tu kuhakiki waliokosa mikopo
wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imetoa muda wa wiki mbili kwa bodi ya mikopo kupitia upya majina ya wanafunzi waliokosa mikopo lakini wakiwa na vigezo vyote vya kupata mikopo
imeshangaza kuona ni idadi ndogo tu ya wanafunzi walioomba mikopo kwa mwaka wa masomo 2011\12 wamefanikiwa kupata mikopo hiyo ikiacha idadi kubwa wakiwa wamekosa. HELSB imekubali kufanya uhakiki huo na bila shaka baada ya wiki mbili tutajua majibu kamili
baadhi ya viongozi HELSB
 kumekua na tetesi kwamba kitendo cha wanafunzi kuandamana kuongezewa kiasi cha fedha ya mkopo ndio chanzo cha waombaji wengi kukosa mkopo sasa, tusubiri majibu ya bodi na sababu zilizofanya idadi kubwa ya waombaji mikopo kwa wakati huu kukosa

Monday, September 5, 2011

Hatma ya wanafunzi wa INTENATIONAL RELATIONS chuo kikuu cha dodoma

Kutokana na migomo ya hapa na pale iliyofanywa na wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma, ililazimu chuo hicho kufungwa na wanafunzi wote wakarudishwa nyumbani wakiambiwa kusubiri hadi watakapoitwa tena chuoni hapo, wanafunzi wa kozi nyingine zote wameitwa kurudi chuo na kuendelea na masomo isipokua wanafunzi wanaosomea INTERNATIONAL RELATIONS kwa madai kuwa wao ndio walikua wachochezi wakubwa wa migomo, swali lagu ni kutaka kujua nini hasa hatma ya wanafunzi hawa??

Tuesday, August 23, 2011

HII NI KWA SJMC STUDENTS...........................

kutakana na sababu siziweza kuzuilika, matokeo ya wanafunzi wa chuo kikuu cha dar es salaam kitivo cha uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma (SJMC) yamekua ya mwisho kutolewa ukilinganisha na vitivo vingine, lakini tatizo hilo lilishashughulikiwa na sasa wanafunzi wa SJMC wanaweza wakayapata matokeo hayo katika mtandao wa ARIS, go and check what you sow guys, skulliz blog wishes you all the luck in the world, love you all

Monday, August 22, 2011

ARIS ARIS ARIS, MATOKEO YAMETOKA

Matokeo ya wanachuo kikuu cha dar es salaam yametoka katika mtandao wa Aris, wanafunzi wote waliofanya mtihani wanashauriwa kuangalia matokeo yao katika mtandao huo, incase kuna tatizo lolote katika matokeo yako, muone class representative wako as soon as possible.
Ninaamini hakuna atakaekua amefanya vibaya sana, na kwa wale wote waliopata sup, poleni sana, jitahidini sana mkasapue izo sup zenu coz hatutaki kuwapoteza chuoni, skulliz blog wishes you all the best

Wednesday, August 10, 2011

YANGA FC, HII NI DHARAU AU TUWAELEWEJE???

 TFF ilitishia kuchukua hatua kali kwa club ya Yanga endapo club iyo ingegoma kuwaruhusu wachezaji wao nane kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars ambayo leo jumatano, siku ya kalenda ya FIFA kwa mechi za kimataifa, inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na sudan huko jijini Khartoum. Yanga imejitetea kuwa walipata mwaliko huo kabla kabla ya wachezaji hao kuitwa timu ya taifa hivyo wana haki ya kuwatumia licha ya ukweli kwamba TFF ina haki zaidi kwani siku hii inatambuliwa na FIFA kwa kuwa ipo kwaenye kalenda ya mechi za timu za taifa na club zinawajibika kuwatoa wachezaji wote wanaoitwa. 
 Sasa Yanga kwa kitendo mlichokifanya kuwazuia wachezaji wenu wasishiriki kuichezea timu yetu ya taifa mnataka watanzania tuwaeleweje, mbona mnakosa uzalendo kiasi hiki??
Kocha wa timu ya taifa, Paulsen imebidi aokote wachezaji ambao hawakua katika list yake, sisemi kama hawana kiwango cha kutosha kuichezea timu yetu ya taifa ila kuna mambo mengi watakua wameyakosa kama kuzoeana uwanjani na mbinu ambazo wachezaji wa siku zote hufundishwa na kocha huyo, hivi timu yetu isipofanya vizuri tumlaumu Paulsen kama tulivofanya kwa Maximo au?
YANGA FC, HII NI DHARAU!!

MHIMBILI UNIVERSITY HAISAJILI TENA WANAFUNZI

Chuo cha mhimbili, MHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES (MUHAS) chafuta udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa kwanza. Inasemekana utawala wa chuo hicho hauna mpango wa kudahili wanafunzi wapya wanaotaka kujiunga chuoni hapo kwa muda wa miaka kadhaa hadi wanafunzi wote waliopo watakapomalizika.
Bado haijajulikana kama lengo la utawala ni kubadili mfumo mzima wa utoaji elimu kwa wanafunzi wapya watakaoanza tena kusoma chuoni hapo au ni kwa ajili ya marekebisho ya majengo ya chuo hicho ambayo kwa kweli hayana mvuto hata kidogo.
Skulliz blog bado inaendelea kufanya uchunguzi ili kupata habari kamili then kama kawa mzigo utadondoshwa hapa hapa live bila chenga, stay tunned brothers n sisterz

Wednesday, August 3, 2011

DIAMOND NA WEMA, Mahaba motomoto, mhm!

kumbe kweli lisemwalo huwa lipo, zilianza tetesi tetesi tu na wenyewe wakakana sana, ooh sisi ni marafiki tu, tupo karibu coz kuna kazi tunafanya pamoja, kumbe kulikua na somethig behind, its good now mmeamua kuweka wazi tu,

diamond na Wema wamechil kimahaaabaaaa





ayayayayayaaaa, jiachieni vijana, Diamond congrats sana naona mtot mzuri kabwaga zake zote kwako,

SERENGETI FIESTA 2011, Aina Majotrooooo

msanii wa kizazi kipya Prof Jay akiwarusha mashabiki ndani ya uwanja wa CCM Kirumba Mwanza

SHAGGY, Msanii wa kimataifa kutoka Jamaica akiwaburudisha mashabiki ndani ya Rock city


mashabiki wakigambeka kitu cha serengeti pale kati, full shangwe


jukwaa la fiesta 2011, ebwanaeee ni noumaa, watu kibaaoooo

Adam Mchomvu, mtangazaji Cloudz fm ndie aliekua MC fiesta ya Mza akiwazingua mashabik kama kawa

msanii Diamond akifanya bonge moja la show, salute kijana

Godzilla, tupe mambo bro.

Ludacris, msanii wa kimataifa from USA akidondosha bonge la show ndani ya viwanja vya leaders, Ludacris ndie aliekua mgeni rasmi fiesta2011, jamaa ni mkali

msanii wa kizazi kipya mwana FA au Binamu akitema rymes, kiufupi fiesta ya mwaka huu ilikua Off da hook, kama hukuweza kuhudhuria trust me, umemic bonge moja la moment