contact


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, September 21, 2011

UKWELI KUHUSU MIGOGORO YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

Kwa takribani miaka minne sasa, kumekuwepo na mvutano kati ya Taasisi ya ustawi wa jamii (ISW) na Baraza la taifa la Elimu ya juu na ufundi (NACTE), kuhusu masuala ya taaluma katika taasisi hiyo. Mvutano huo uliwasukuma baadhi ya wahadhiri katika taasisi hiyo kushinikiza menejimenti yao kutekeleza mapendekezo ya baraza hilo kuboresha taaluma, lakini kilichowakuta wahadhiri hao, licha ya juhudi zote zilizofanywa na vyombo mbalimbali kujaribu kurekebisha mambo katika taasisi hiyo, bodi ya chuo iliridhia kuwafukuza kazi wahadhiri 21 mnamo agosti 21 mwaka huu, ambao kosa lao pekee kubwa ni kutaka taaluma iboreshwe katika chuo hicho

Wahadhiri hao wamefukuzwa kwa madai kwamba waliendesha mgomo usio halali na kukaidi maagizo ya mamlaka za juu


Mambo bado si shwari katika taasisi hiyo, mpaka sasa hakuna maboresho yoyote ya maana ya kitaaluma yaliyofanyika,  bali kinachoendelea pale ni migogoro ambayo hatma yake ni kuzalisha wahitimu walio chini ya kiwango wasioweza kushindana vyema katika soko gumu la ajira nchini


Ukweli ni kwamba, kiini cha migogoro ni taasisi kuendelea kupuuza maagizo ya NACTE. kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba barua za NACTE zenye kumbukumbu NACTE/ DA/ 31/655/Vol 1./92 ya june 19/ 19/ 2010; zinaonyesha taasisi ya ustawi wa jamii ilipewa maagizo ya kufanya maboresho ili kukidhi matakwa ya ithibati yanayokubalika NACTE

Kwa mshangao, menejimenti iliamua kukaidi maagizo hayo ya NACTE. Na hili ndilo pia lililosababisha wahadhiri watatu waandamizi wa chuo hicho -Dk Mihanja, Dk Matiku na Dk Kitojo kujiuzulu kazi mwaka 2007.


Ukaidi huo ulisababisha taasisi kuzuiliwa kujihusisha na udahili wa programu za ngazi ya cheti, stashahada na shahada (certificate, diploma, degree programs) ilipofika April 2011, kwa kuwa ilishindwa kukidhi matakwa ya ithibati ya kwanza iliyoidhinishwa na NACTE kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2006-2011


Kwa barua hizo taasisi ilipewa muda mpya wa kuandaa mitaala na kurekebisha mfumo wa utawala hadi ifikapo septemba 2011 ili warudishiwe haki ya kuendesha program hizo, mpaka wiki mbili zilizopita hilo lilikuwa halijatendeka

Kwa ufupi, si kweli kwamba tatizo la taasisi hiyo lilikua ni hao wadhahiri waliofukuzwa kazi kama inavyodaiwa, wao walikuwa wakipigania taasisi hiyo kutii maagizo yaliyotolewa na NACTE. Si kweli kwamba waliachishwa kazi kwa kufanya mgomo usio halali, na si kweli kwamba kwa kuwafukuza kazi, hali ya kitaaluma ya taasisi hiyo itaboresheka,  ni mpaka hapo hilo litakapozingatiwa, hali ya kitaaluma ya taasisi hiyo haiwezi kuwa shwari, kwa sababu wahitimu wa taasisi hiyo wataendelea kuwa chini ya viwango na ajira zitaendelea kuwakimbia


menejimenti ya taasisi hiyo imekiuka haki za msingi za wafanyakazi walioachishwa kazi bila kufuata kanuni za ajira za taasisi ya ustawi wa jamii (staff regulation) na sheria ya kazi Na.6 ya mwaka 2004, na kwa mujibu wa katiba ya nchi, pia imewadhalilisha wadhahiri hao walioachishwa kazi wakipigania maslahi ya taasisi, maslahi ya wanafunzi na maslahi ya umma mzima wa Tanzania

Monday, September 19, 2011

SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA LATEKETEA KWA MOTO

Mbunge wa Mbeya mjini, Mh Joseph Mbilinyi aka Sugu akiwa ametembelea soko la SIDO mwanjelwa jijini Mbeya likiwa linateketea kwa moto

Moto ukizidi kupamba katika soko la mwanjelwa Mbeya mjini,  raia wakikimbia kuokoa maisha yao na wengine wakikimbilia eneo la tukio kuokoa chochote kinachowezekana, chanzo cha moto huu hakijajulikana mpaka sasa

Mabanda ya soko yakiteketea, kikosi cha kuzima moto cha jiji hili kilifika eneo la tukio kuzima moto na kuokoa watu na mali zao kikiwa na gari bovu na pia likiwa halina maji ya kuzimia moto huu

AJALI YA MELI ZANZIBAR

abiria wa meli ya MV Spice Islander ilyopata ajali usiku wa kuamkia septemba 10,2011 ikiwa inaelekea Pemba  kutokea Dar es salaam wakijitahidi kuokoa uhai kwao kwa kutumia magodoro yaliyokuwamo katika meli hiyo

Muonekano wa nje wa meli ya MV Spice Islander kabla ya kupata ajali, meli hii inasemekana ilibeba abiria zaidi ya 1500, idadi ambayo ni zaidi  ya mara mbili ya idadi ya abiria inayopaswa kubeba

Baadhi ya miili ya abiria iliyopatikana katika ajali hiyo, mamia ya watu wamepoteza uhai katika ajali hii

Baadhi ya wahanga wa ajali hii waliofanikiwa kuokolewa

Makaburi yaliyochimbwa Zanzibar kwa ajili ya kuwazika marehemu wa ajali ya meli

Meli ya MV Spice ikiwa imepinduka maeneo ya Nungwi, meli hii iliondoka bandari Zanzibar kuelekea jioni ya tarehe 9 septemba, ilianza kuzama mida ya saa 3 usiku na hatimaye kupinduka  na kuzama kabisa, meli hii ilielemewa na mizigo na idadi kubwa ya abiria

Askari na raia wakijitahidi kuokoa abiria waliosalimika katika ajali hiyo, kikosi cha jeshi la polisi wanamaji KMKM na JKU bado vinaendelea na utafutaji wa miili ya abiria wengine wa ajali hiyo

muonekano  wa meli ya MV spice ikiwa inaendelea kuzama ndani ya maji

Baadhi ya miili ya watoto wadogo waliopoteza maisha katika ajali ya meli

Ndugu na jamaa wakiwaombea watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli Zanzibar. hii ni meli ya pili kuzama ikielekea Pemba, nyingine ni MV Fatahi iliyozama mwaka jana ikiwa bandari zanzibar kuelekea Pemba

Friday, September 9, 2011

MAMILIONI KUMWAGIKA KISIWANI KILWA

shehemu ya mabaki ya kilwa
 Sept 7, 2011 serikali ya Marekani kupitia balozi wake nchini imewasilisha msaada wa (1,132,000,000.00) shilingi za kitanzania, karibia bilioni moja na robo kusaidia utunzaji wa hifadhi za kumbukumbu za Kilwa
ufukwe wa bahari, Kilwa
 Hifadhi hizo  ambazo zimekuwepo tangu karne ya 19 zinatakiwa kutunzwa ili ziendelee kuwa kivutio kizuri cha utalii nchini na kuingizia taifa kipato zaidi. Msaada huo uliopita chini ya US Department of State's Ambassadors Fund for Cultural Preservation (AFCP) umetolewa kwa lengo la kusaidia utunzaji wa hifadhi za mambo ya kale Africa Mashariki na pia kuwawezesha wakazi wa maeneo hayo kunufaika na hifadhi hizo
sehemu ya mabaki ya Kilwa

NIGER KUMSHUGHULIKIA GADDAFI

Col. Muammar Gaddafi
 Serikali ya Niger imesema kuwa itaamua jinsi ya kushughulika na kanali Muamar Gaddafi iwapo ataingia nchini humo kuomba hifadhi ya kisiasa
Kanali Muamar Gaddafi
Ripoti kutoka eneo hilo zimesema maofisa wa  vyeo vya juu katika serikali iliyotimuliwa wamewasili nchini Niger na kuna habari kuwa huenda Gaddafi akajiunga nao. Baraza la mpito la Libya limetoa wito kwa serikali ya Niger isimpe hifadhi kanali Gaddafi
Kanali Gaddafi na walinzi wake wa kike
 wakati huo huo Kanali Gaddafi amepuuza madai kwamba ametorokea nchi jirani ya Niger na kuyataja madai hayo kama uongo  na vita vya kiakili. Matamshi ya Gaddafi yamepeperushwa na kituo kimoja cha TV nchini Sirya kilichodai kuwa Kanali Gaddafi bado yupo nchini Libya. Gaddafi ameapa  kuwashinda wapiganaji wa upinzani wanaoungwa mkono na majeshi ya NATO. Huu ni ujumbe  wake wa kwanza katika kipindi kirefu
Walinzi wa Kanali Gaddafi
.
Baraza la kitaifa la mpito la Libya limetoa wito kwa Niger kutompa hifadhi Kanali Gaddafi. Serikali ya  Niger imesema kwamba itaamua yenyewe jinsi itakavyomshughulikia Gaddafi ikiwa ataingia nchini humo

OBAMA kuwekeza katika elimu tena, KIKWETE......??

raisi Barrack Obama
 Raisi wa marekani Barrack Hussein Obama amewasilisha mpango unaoazimia kufufua uchumi na kutoa nafasi mpya za ajira utakaogharimu dola za kimarekani billion 450
Katika hotuba yake iliyokua ikingojewa kwa hamu, Obama ameliambia bunge la marekani, lengo ni kufufua uchumi wa marekani uliozorota, kutoa nafasi mpya za ajira na kuwapa vijana matumaini
Kiini cha mpango huo ni kupunguza gharama za ruzuku ya serikali kwa wale wasiojiweza na kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu na miundo mbinu, pia ameongeza kuwa atabadilisha mfumo wa kodi uwe ni wa haki kwa kila mmoja
rais Jakaya Kikwete
Raisi wetu kikwete tungependa uige mifano kama hii, kodi  sawa kwa wwote, rasilimali ziwasaidie wananchi wa hali zote na sio wanaojiweza tu na kikubwa zaidi ni kuwekeza katika elimu, walimu ni wachache nao pia kila kukicha wanalalamika mishahara haiwatoshelezi mahitaji yao, wanafunzi wa vyuo vikuu wanagoma kila kukicha wakidai  mikopo, shule  za kata nyingi lakini vitabu hakuna, wakati huo huo mshahara wa mbunge kwa mwezi ni sawa na mshahara  wa mwalimu wa kawaida kwa mwaka mzima

WANAFUNZI WAVAMIA OFISI ZA TCU

wanafunzi wakiwa katika maandamano
 mamia ya wanafunzi ambao hawakuchaguliwa na tume ya vyuo vikuu (TCU) kujiunga na vyuo vikuu nchini juzi walivamia ofisi za tume hiyo ili kufahamu sababu za kutochaguliwa kwao licha ya kuwa na vigezo na sifa zote zinazotahitajika ili kuchaguliwa
wanafunzi wakiwa katika maandamano
Vijana hao ni miongoni mwa wanafunzi 10,553 ambao hawakuchaguliwa kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka huu. Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa na TCU kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka huu imepungua ukilinganisha na ile ya mwaka jana, 

BODI YA MIKOPO KUCHUNGUZA TENA UTOAJI WA MKOPO KWA WALIOKOSA

bodi ya mikopo elimu ya juu
Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu Tanzania (HELSB) imepewa muda wa wiki mbili tu kuhakiki waliokosa mikopo
wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imetoa muda wa wiki mbili kwa bodi ya mikopo kupitia upya majina ya wanafunzi waliokosa mikopo lakini wakiwa na vigezo vyote vya kupata mikopo
imeshangaza kuona ni idadi ndogo tu ya wanafunzi walioomba mikopo kwa mwaka wa masomo 2011\12 wamefanikiwa kupata mikopo hiyo ikiacha idadi kubwa wakiwa wamekosa. HELSB imekubali kufanya uhakiki huo na bila shaka baada ya wiki mbili tutajua majibu kamili
baadhi ya viongozi HELSB
 kumekua na tetesi kwamba kitendo cha wanafunzi kuandamana kuongezewa kiasi cha fedha ya mkopo ndio chanzo cha waombaji wengi kukosa mkopo sasa, tusubiri majibu ya bodi na sababu zilizofanya idadi kubwa ya waombaji mikopo kwa wakati huu kukosa

Monday, September 5, 2011

Hatma ya wanafunzi wa INTENATIONAL RELATIONS chuo kikuu cha dodoma

Kutokana na migomo ya hapa na pale iliyofanywa na wanafunzi wa chuo kikuu cha dodoma, ililazimu chuo hicho kufungwa na wanafunzi wote wakarudishwa nyumbani wakiambiwa kusubiri hadi watakapoitwa tena chuoni hapo, wanafunzi wa kozi nyingine zote wameitwa kurudi chuo na kuendelea na masomo isipokua wanafunzi wanaosomea INTERNATIONAL RELATIONS kwa madai kuwa wao ndio walikua wachochezi wakubwa wa migomo, swali lagu ni kutaka kujua nini hasa hatma ya wanafunzi hawa??