contact


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Monday, February 13, 2012

sababu za kifo cha Whitney

hadi sasa kifo cha mwanamuziki maarufu whitney houston bado kimebaki kuwa fumbo gumu kwani bado chanzo cha kifo chake hakijajulikana, police wa beverly hillz ambako  nndipo alipofia mwanadada huyo  wanasema taarifa kamili itatolewa baada ya majibu ya uchunguzi wa mwili wa mwanamuziki huyo (toxcology) yatapotoka, uchunguzi huo unaweza kuchukua muda wa wiki 12 hadi 16.
Ripoti nyingine kutoka kwa watu wa karibu na wanafanyakazi wa hoteli aliyofia mwanadada huyo zinasema Whitney alikufa ndani ya sink la kuogea (bathtub) lakini hakufa kwa kuzama na maji na hii ni kwa kuwa uchunguzi unaonyesha mapafu ya mwanadada huyo hayakua na maji, pia inasemekana kulipatikana makopo kadhaa ya vidonge kama amoxcilin, xanax na mengineyo ambayo inasadikika kuwa ndio chanzo cha kifo  cha mwanadada huyo, mcahanganyiko wa dawa hizo pamoja na kilevi vinasemekana kumsababishia mshituko wa moyo na kuchukua uhai wa mwanadada huyo
Marehemu Whitney aliezaliwa mwaka 1963 na kufariki 2012 anategemewa kuzikwa ijumaa hii 17 feb 2012 huko prudential centre Newark