contact


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Thursday, November 24, 2011

MIGOMO SIO ISHU

Kwa mtazamo wangu kiukweli mimi sioni faida ya migomo no matter tunapigania kitu gani, hii ni kutokana na mambo yaliotokea hapa juzikati, baaadhi ya wanafunzi wameumizwa kwa kupigwa na askari, wengine tumeumizwa na mabomu ya machozi, hii sio mara ya kwanza kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kugoma na kuandamana, kama kweli migomo ingekua inasaidia, haya matatizo yasingekua yanajirudia, tutaendelea kupigwa mabomu ya machozi na mwisho wa siku tutakuja kupigwa hata na risasi za moto na matatizo yataendelea kujirudia kama kawa, me nashauri tungejaribu kutafuta njia nyingine ya kuwafanya hawa viumbe watuelewe, kuna wanafunzi wa mwaka wa kwanza pia wameandamana, nyie hamjafikisha hata semista moja hapa chuo mmeshaanza kujiingiza matatizoni, mkiumizwa au kufukuzwa chuo mtawaelezea habari gani wazazi wenu ambao wanajinyima ili nyie mpate elimu, acheni kufata mkumbo wadogo zangu, someni, hicho ndicho kilichowaleta UDSM.

Friday, November 4, 2011

CHUO CHA MAENDELEO NA USIMAMIZI WA MAJI (WDMI)

          Jina chuo cha maendeleo na usimamizi wa maji linaweza kuwa geni masikioni mwa watu, lakini chuo hichi ni moja kati ya vyuo vikongwe hapa nchini, kilianzishwa mwaka 1974 kikijulikana kama RWEGALULILA WATER RESOURCE INSTITUTE, dhumuni kubwa ikiwa ni wataalam katika fani mbalimbali zinazohusu MAJI.
         Kubadilika kwa jina na kuwa WATER DEVELOPMENT AND MANADEMENT INSTITUTE, ilifanyika mwaka 2008, baada ya chuo kupewa hadhi ya kuwa wakala wa serikali yaani Agency, mpaka sasa chuo kinatoa kozi tano katika ngazi ya Diploma, WATER SUPPLY AND SANITATION ENGINEERING, HYDOGEOLOGY AND WATER WELL DRILLING. HYDROLOGY AND METROLOGY, WATER LABORATORY TECHNOLOGY na IRRIGATION ENGINEERING. Mipango ya degree kuanza imekamilika na muda wowote WATER RESOURCE AND IRRIGATION ENGINEERING  itaanza, sasa kazi kwenu nyie wenye hamu ya kufanya kazi kwenye sekta ya maji, mnakaribishwa sana.

Monday, October 24, 2011

WANACHUO SJMC KUANDAMANA BODI YA MIKOPO LEO

Licha ya wanafunzi kupiga kelele kibao na migomo ya hapa na pale kuielekea bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania, bodi hiyo inaonyesha live kutozingatia kwa kuendelea kuchelewesha mikopo ya wanafunzi. Hii inatokana na wanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma (sjmc) kutopata mkopo wao hadi leo, Wanafunzi wa chuo hicho sasa hivi wameamua kwenda bodi ya mikopo ili wakapate kujua ni ishu gani inaendelea na kwanini haya matatizo hayaishi, ni uzembe tu wa wafanyakazi au inakuaje, tunakoelekea kama tatizo hili litaendelea itakua balaa, Bodi kaeni chonjo mmeshatuchosha

Wednesday, September 21, 2011

UKWELI KUHUSU MIGOGORO YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII

Kwa takribani miaka minne sasa, kumekuwepo na mvutano kati ya Taasisi ya ustawi wa jamii (ISW) na Baraza la taifa la Elimu ya juu na ufundi (NACTE), kuhusu masuala ya taaluma katika taasisi hiyo. Mvutano huo uliwasukuma baadhi ya wahadhiri katika taasisi hiyo kushinikiza menejimenti yao kutekeleza mapendekezo ya baraza hilo kuboresha taaluma, lakini kilichowakuta wahadhiri hao, licha ya juhudi zote zilizofanywa na vyombo mbalimbali kujaribu kurekebisha mambo katika taasisi hiyo, bodi ya chuo iliridhia kuwafukuza kazi wahadhiri 21 mnamo agosti 21 mwaka huu, ambao kosa lao pekee kubwa ni kutaka taaluma iboreshwe katika chuo hicho

Wahadhiri hao wamefukuzwa kwa madai kwamba waliendesha mgomo usio halali na kukaidi maagizo ya mamlaka za juu


Mambo bado si shwari katika taasisi hiyo, mpaka sasa hakuna maboresho yoyote ya maana ya kitaaluma yaliyofanyika,  bali kinachoendelea pale ni migogoro ambayo hatma yake ni kuzalisha wahitimu walio chini ya kiwango wasioweza kushindana vyema katika soko gumu la ajira nchini


Ukweli ni kwamba, kiini cha migogoro ni taasisi kuendelea kupuuza maagizo ya NACTE. kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kwamba barua za NACTE zenye kumbukumbu NACTE/ DA/ 31/655/Vol 1./92 ya june 19/ 19/ 2010; zinaonyesha taasisi ya ustawi wa jamii ilipewa maagizo ya kufanya maboresho ili kukidhi matakwa ya ithibati yanayokubalika NACTE

Kwa mshangao, menejimenti iliamua kukaidi maagizo hayo ya NACTE. Na hili ndilo pia lililosababisha wahadhiri watatu waandamizi wa chuo hicho -Dk Mihanja, Dk Matiku na Dk Kitojo kujiuzulu kazi mwaka 2007.


Ukaidi huo ulisababisha taasisi kuzuiliwa kujihusisha na udahili wa programu za ngazi ya cheti, stashahada na shahada (certificate, diploma, degree programs) ilipofika April 2011, kwa kuwa ilishindwa kukidhi matakwa ya ithibati ya kwanza iliyoidhinishwa na NACTE kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2006-2011


Kwa barua hizo taasisi ilipewa muda mpya wa kuandaa mitaala na kurekebisha mfumo wa utawala hadi ifikapo septemba 2011 ili warudishiwe haki ya kuendesha program hizo, mpaka wiki mbili zilizopita hilo lilikuwa halijatendeka

Kwa ufupi, si kweli kwamba tatizo la taasisi hiyo lilikua ni hao wadhahiri waliofukuzwa kazi kama inavyodaiwa, wao walikuwa wakipigania taasisi hiyo kutii maagizo yaliyotolewa na NACTE. Si kweli kwamba waliachishwa kazi kwa kufanya mgomo usio halali, na si kweli kwamba kwa kuwafukuza kazi, hali ya kitaaluma ya taasisi hiyo itaboresheka,  ni mpaka hapo hilo litakapozingatiwa, hali ya kitaaluma ya taasisi hiyo haiwezi kuwa shwari, kwa sababu wahitimu wa taasisi hiyo wataendelea kuwa chini ya viwango na ajira zitaendelea kuwakimbia


menejimenti ya taasisi hiyo imekiuka haki za msingi za wafanyakazi walioachishwa kazi bila kufuata kanuni za ajira za taasisi ya ustawi wa jamii (staff regulation) na sheria ya kazi Na.6 ya mwaka 2004, na kwa mujibu wa katiba ya nchi, pia imewadhalilisha wadhahiri hao walioachishwa kazi wakipigania maslahi ya taasisi, maslahi ya wanafunzi na maslahi ya umma mzima wa Tanzania

Monday, September 19, 2011

SOKO LA SIDO MWANJELWA MBEYA LATEKETEA KWA MOTO

Mbunge wa Mbeya mjini, Mh Joseph Mbilinyi aka Sugu akiwa ametembelea soko la SIDO mwanjelwa jijini Mbeya likiwa linateketea kwa moto

Moto ukizidi kupamba katika soko la mwanjelwa Mbeya mjini,  raia wakikimbia kuokoa maisha yao na wengine wakikimbilia eneo la tukio kuokoa chochote kinachowezekana, chanzo cha moto huu hakijajulikana mpaka sasa

Mabanda ya soko yakiteketea, kikosi cha kuzima moto cha jiji hili kilifika eneo la tukio kuzima moto na kuokoa watu na mali zao kikiwa na gari bovu na pia likiwa halina maji ya kuzimia moto huu

AJALI YA MELI ZANZIBAR

abiria wa meli ya MV Spice Islander ilyopata ajali usiku wa kuamkia septemba 10,2011 ikiwa inaelekea Pemba  kutokea Dar es salaam wakijitahidi kuokoa uhai kwao kwa kutumia magodoro yaliyokuwamo katika meli hiyo

Muonekano wa nje wa meli ya MV Spice Islander kabla ya kupata ajali, meli hii inasemekana ilibeba abiria zaidi ya 1500, idadi ambayo ni zaidi  ya mara mbili ya idadi ya abiria inayopaswa kubeba

Baadhi ya miili ya abiria iliyopatikana katika ajali hiyo, mamia ya watu wamepoteza uhai katika ajali hii

Baadhi ya wahanga wa ajali hii waliofanikiwa kuokolewa

Makaburi yaliyochimbwa Zanzibar kwa ajili ya kuwazika marehemu wa ajali ya meli

Meli ya MV Spice ikiwa imepinduka maeneo ya Nungwi, meli hii iliondoka bandari Zanzibar kuelekea jioni ya tarehe 9 septemba, ilianza kuzama mida ya saa 3 usiku na hatimaye kupinduka  na kuzama kabisa, meli hii ilielemewa na mizigo na idadi kubwa ya abiria

Askari na raia wakijitahidi kuokoa abiria waliosalimika katika ajali hiyo, kikosi cha jeshi la polisi wanamaji KMKM na JKU bado vinaendelea na utafutaji wa miili ya abiria wengine wa ajali hiyo

muonekano  wa meli ya MV spice ikiwa inaendelea kuzama ndani ya maji

Baadhi ya miili ya watoto wadogo waliopoteza maisha katika ajali ya meli

Ndugu na jamaa wakiwaombea watu waliopoteza maisha katika ajali ya meli Zanzibar. hii ni meli ya pili kuzama ikielekea Pemba, nyingine ni MV Fatahi iliyozama mwaka jana ikiwa bandari zanzibar kuelekea Pemba

Friday, September 9, 2011

MAMILIONI KUMWAGIKA KISIWANI KILWA

shehemu ya mabaki ya kilwa
 Sept 7, 2011 serikali ya Marekani kupitia balozi wake nchini imewasilisha msaada wa (1,132,000,000.00) shilingi za kitanzania, karibia bilioni moja na robo kusaidia utunzaji wa hifadhi za kumbukumbu za Kilwa
ufukwe wa bahari, Kilwa
 Hifadhi hizo  ambazo zimekuwepo tangu karne ya 19 zinatakiwa kutunzwa ili ziendelee kuwa kivutio kizuri cha utalii nchini na kuingizia taifa kipato zaidi. Msaada huo uliopita chini ya US Department of State's Ambassadors Fund for Cultural Preservation (AFCP) umetolewa kwa lengo la kusaidia utunzaji wa hifadhi za mambo ya kale Africa Mashariki na pia kuwawezesha wakazi wa maeneo hayo kunufaika na hifadhi hizo
sehemu ya mabaki ya Kilwa